Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Mbweni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar leo tarehe 08 Januari, 2026.