Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Karibu

Karibu kwenye Tovuti rasmi ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali  ya Tanzania. Ofisi hii inatambua kuwa  unategemea taarifa sahihi  katika utambuzi na uvumbuzi wa mawazo mapya ya kuimarisha Sera na mwenendo bora.  Tovuti hii imetayarishwa ili  kukurahisishia kupata  taarifa bure kuhusu shughuli za kila siku za Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi zinazoboreshwa mara kwa mara.

Kwa kuzingatia dhamira ya Katibu Mkuu Kiongozi ya kutaka taarifa sahihi za kazi ya kuwahudumia wananchi zipatikane kwa urahisi na kwa wakati kwa watu wa kawaida, Asasi mbalimbali zisizo za Serikali, Kitaifa na Kimataifa na watoa maamuzi ya kisera . Wakati huo huo kuwahakikishia wananchi usalama na faragha.

Tovuti hii pia imetayarishwa kwa namna rahisi ya kupata rasilimali zaidi, zana bora, na picha za kawaida za kusaidia  kazi yako. Tunakaribisha maoni yako kuhusu Tovuti hii  au masuala mengine ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi.