Mwenyekiti wa AAAPM Tawi la Tanzania, Bi. Leila Mavika akitoa maelezo mafupi kuhusu AAPAM Tawi la Tanzania kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kabla ya kufunga Mkutano wa 11 wa Wanachama wa AAPAM Tawi la Tanzania leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) tarehe 4 Mei,2024.